Faida saba za kutumia lugha sanifu

Lugha ni nyenzo kubwa sana katika mawasiliano ya kila siku katika jamii. Lugha imewezesha mambo mengi sana akatika jamii zetu kote duniani. Lugha imesaidia sana katika nyanja mbalimbali ikiwemo upashanaji habari,elimu, kusambaza teknolojia na hata kuburudisha. Lugha inatakiwa kutumiwa kwa usahihi kulingana na muktadha mada husika na wazungumzaji pia. Kila jamii ina lugha yake na hakuna lugha iliyo bora kuliko lugha nyingine. Kutokujua matumizi sahihi ya lugha unayoitumia husababisha madhara makubwa katika mawasiliano ya kila siku.Mathalan utumiaji mbovu wa maneno,uandishi usio sahihi na hata matamshi mabovu ni makosa makubwa ambayo hufanywa kila siku na watumiaji wa lugha husika, hivyo kupelekea kutoa ujumbe tata kwa mlengwa/walengwa wako. Katika lugha ya uandishi vituo pia ni muhimu mfano nukta,mkato,alama ya kuuliza nk.

1.Kufikisha ujumbe uliokusudiwa kwa usahihi
Ili uweze kueleweka kwa urahisi ni muhimukutumia maneno yote ya lugha husika kwa usahihi bila kubadili matamshi ama maandishi sahihi ya maneno ili
kuweza kufikisha ujumbe uliokusudiwa kwa mlengwa. Mathalani kutumia ufupisho wa maneno usioeleweka,matamshi mabovu mfano matamshi kulingana  na lugha mama ambayo mara nyingi kwa kiswahili ni na z,th na dh,r na l ambayo mara nyingi huleta mkanganyiko kwa msikilizaji. Hili tatizo hutokana zaidi na lugha za makabila na mazingira ya kuishi. Haya huwafanya baadhi ya watu kutokujua ni wapi pa kuweka maneno hayo kw usahihi na kuonekana kana kwamba hawaijui lugha husika. Pia matumizi ya mitandaoyamewafanya watu wengi kutumia lugha fupi (text language) ambayo yamewaathiri katika matumizi sahihi ya maneno mfano herufi watu wengi wamekuwa wakiiondoa ama kuiweka sehemu isiyo sahihi, mfano atawakuta akiwa na maana ya