Faida za kiafya zitokanazo na ulaji wa ndizi mbivu

Ndizi mbivu ni tunda lilotokanalo na mmea wa mgomba. Katika nchi yetu ya Tanzania kuna mikoa ambayo imebarikiwa kuzalisha ndizi kwa wingi. Mikoa hiyo ni Arusha, Kagera, Kilimanjaro, Mbeya na Morogoro. Ndizi zina rangi ya kijani zinapokuwa mbichi na njano zinapoiva na hivyo kuwa na rangi ya kuvutia. Ndizi pia zina ukubwa na maumbo tofauti tofauti. Ndizi mbichi hutumika kwa chakula kwa kupikwa na kuchanganywa na vyakula vingine kama nyama, maharage na samaki ila zikivumbikwa na kuiva hutumika kama tunda. Baadhi ya makabila hutumia ndizi mbivu kutengeneza pombe za asili kama lubisi na mbege. Pia kuna viwanda vya kisasa vinavyotumia ndizi kutengeneza mvinyo (wine). Kuna aina nyingi za ndizi lakini faida zake mwilini zinafanana.

Zipo faida kadhaa zinazotokana na ulaji wa ndizi mbivu. Faida hizo ni kama kudhibiti kiasi cha sukari mwili na pia kufanya mwili kutengeneza kemikali maalum za kufanya mwili kupumzika/kupunguza msongo. Faida nyingine ya ndizi mbivu ni uwezo wake wa kuweza kupunguza uvimbe katika sehemu ya mwili, kuzuia aina ya pili ya kisukari (type II diabetes), kupunguza uzito hasa kwa kuwa ndizi zina kiwango kikubwa cha nyuzi nyuzi (fibres), kuimarisha mfumo wa fahamu na kusaidia katika utengenezajiwa chembe nyeupe za damu (white blood cells) ambazo hupambana na magonjwa mwilini hasa kutokana na kuwa na kiwango kikubwa cha vitamini B-6.
SOMA: Namna bora ya kupungiuza uzito
Pia ndizi mbivu husaidia kupunguza sononeko (depression) kutokana na kuwa na kiwango kikubwa cha tryptophan ambayo hubadilishwa kuwa serotinin ambayo ni kihamasishi cha kutoa furaha katika ubongo. Mbali na faida hizo ndizi huoingeza nishati mwili kwa kuwa na wanga na sukari, huongeza damu kwa kuwa na madini ya chuma na hivyo kukuepusha na ugonjwa wa upungufu wa damu maarufu kama anaemia. Ndizi pia husaidia pia katika umeng`enyaji wa chakula (digestion) na kusaidia kupambana na sumu ziingiazo mwili kupitia vyakula mbalimbali.
Faida zingine zinazotokana na tunda hili maarufu ni husaidia kuupa utumbo afya kwa kuruhusu kuzaliana kwa bakteria wazuri ambao hufanya kazi mbalimbali mwili maarufu kama prebiotiki na husaidia pia katika utengenezaji wa vimeng`enyo kwaajili ya umeng`enyaji wa chakula mwilini. Kama vile haitoshi ndizi pia husaidia pia kupunguza maumivu ya vidonda vya tumbo kwa kufunika utumbo dhidi ya tindikali zichubuazo utumbo kama Haidrokloriki. Ndizi hutumika kupambana na kemikali zisizotakiwa mwilini au sumu (antiodixants) na pia kupambana na baadhi ya magonjwa sugu. Ndizi zina kiwango kikubwa cha madini ya magneziam na vitamini B ambayo husaidia kuacha uvutaji wa sigara.

Faida zingine ambazo hutokana na ndizi ni kusaidia afya ya akili hasa kumbukumbu na kujifunza, kusaidia tumbo kufanya kazi vizuri kutokana na kuwa na kiwango kikubwa cha cha nyuzi nyuzi (fibres), kupunguza kichefuchefu na kusaidia afya ya macho kwa kuzuia uharibifu wa misuli ya macho .Pia ndizi huzuia saratani ya figo na kuimarisha mifupa hasa kutokana na kuongeza uwezo wa mwili kuchukua madini ya kalsham kutoka kwenye vyakula vingine. Mwisho ndizi husaidia kurudisha chumvichumvi na sukari ipoteayo mwilini kutokana na ugonjwa wa kuendesha (diarrhea).
Naamini kuanzia sasa utaongeza ulaji wako wa ndizi mbivu ili kupata faida hizo zaidi ya kumi nilizoziainisha hapo juu. Kumbuka nyumba hujengwa kwa tofali, miti na zege lakini mwili wenye afya njema hujengwa kula vyakula bora.
Usisahau kumshirikisha mwenzako.
Makala hii imeandaliwa na kuandikwa na:
Nickson Yohanes
nmyohanes@gmail.com

Madhara ya kutumia mifuko ya plastiki (rambo) kubebea vyakula vya moto

Habari za wakati huu ndugu msomaji wa makala zangu katika mtandano huu wa PAMBAZUKA DAIMA ni matumaini yangu kwamba uko bukheri wa afya, na kama kwa vyovyote vile hali yako ya kiafya siyo ya kuridhisha basi nakupa pole na kukuombea upate nafuu na upone haraka.

Ndugu msomaji kumekuwepo na tabia ya watu wengi kupuuzia vitu ambavyo vina madhara kidogo ama ambavyo huchukua muda mrefu kuliko vile ambavyo vinaonyesha madhara katika muda mfupi. Vitu ambavyo vinasababisha ugonjwa papo hapo ama baada ya muda mfupi huchukuliwa kwa umakini mkubwa kulinganisha ni vile ambavyo vinachukua muda mrefu kusababisha ugonjwa.


Leo ningependa kidogo kuzungumzia vifungashio (packages) vya vya chakula ambavyo vimekuwa vikitumiwa na wetu wengi hasa kubebea vyakula vya moto kama chipsi. Vifungashio hivyo si vingine bali ni mifuko ya plastiki maarufu kama mifuko ya rambo. Ukiangalia kwa jicho la kawaida hutaweza kuona madhara yake moja kwa moja hasa kutokana na kwamba huchukua muda mrefu kuja kuona madhara yake ni hivyo watu wengi kutokutilia maanani na mazoea pia ya matumizi ya mifuko hiyo kwenye jamii zetu.

Mitaani na maeneo hasa ya vyuo vikuu kumekuwa na mazoea ya kubeba vyakula vya moto hasa chipsi wakiwa na lengo la kwenda kulia sehemu nyingine mbali na sehemu vinapouzwa.
Mifuko ya plastiki inapopigwa na joto mkali au mdogo kwa muda mrefu hutoa kemikali ambazo huingia kwenye chakula na hivyo kuingizwa mwilini kwa njia ya kula. Kama kemikali hizo zitaendelea kuingizwa kwenye mwili zitaendelea kujijenga mwilini na hivyo kumuweka mlaji katika hatari ya kuugua ugonjwa wa saratani (kansa). Ugonjwa wa kansa kama mjuavyo hauwezi kuanza kama malaria bali huanza kidogo kidogo na mpaka uje kuonekana basi utakuwa umeshambaa sana mwilini. Hatari iliyopo katika mifuko hii si kwa vyakula vya baridi bali vyakula vya moto ambavyo hufanya kemikali hizo kuyeyuka na kuingia kwenye chakula. Kemikali hizo zinajulikana kama Polyvinyl Chloride, polyethylene, polystyrene, styrene na bisphenol.

Mbali na kuongeza uwezekano wa kuugua saratani pia madhara mengine yanayohusishwa na matumizi ya mifuko ya plastiki kubebea vyakula vya moto ni kubadilika kwa jeni za mwili, kuharibika kwa jeni za mwili, matatizo ya uzazi, matatizo ya moyo na matatizo ya kushindwa kuweka katika msawazo (urari) vichocheo mbalimbali vya mwili (homoni) ambavyo husaidia ufanyaji bora kazi wa mwili na hivyo kuathiri baadhi ya tabia hasa kwa watoto.

Kama hakuna ulazima wa wewe kutumia mifuko ya plastiki kubebea vyakula vya moto basi acha kabisa maana matumizi yake. Wahenga walisema ´bora kinga kuliko tiba´, hivyo basi ni bora kuzuia tatizo linalozuilika sasa ili kuepuka madhara ya kesho. Ni imani yangu kwamba utaweza kupunguza matumizi ya mifuko ya rambo katika kubebea vyakula vya moto na hatimae kuacha kabisa. Najua sio jambo rahisi hasa kama umeshazoea lakini ukiamua utaweza kabisa kuacha matumizi hayo.
Nikutakie utekelezaji mwema.

Nickson Yohanes
Email: nmyohanes@gmail.com

Wanaobebeshwa lawama hizi, hawastahili kuzibeba

Malezi kwa watoto yamekuwa changamoto kubwa sana katika dunia hii ya sayansi na teknolojia tena dunia inayokwenda kwa kasi sana mithili ya roketi, dunia iliyojaa kila aina ya changamoto. Imekuwa ni kawaida sasa kusikia watu wazima wakiwalalamikia vijana ama watoto kuwa wamekuwa na tabia ambazo si nzuri hasa kulinganisha na wakati wao. Siwapingi lakini nani wa kulaumiwa, je mtoto, mzazi au jamii?.


Kabla sijamtaja mtu wa kulaumiwa (japo sishauri hivyo) nikumbushe kuwa mtoto huzaliwa akijua vitu viwili tu kulia na kunyonya na kuanzia hapo huanza kujifunza kidogo kidogo hasa kwa picha ama matendo. Baadae ataanza kujifunza maneno afikapo umri wa kuongea na hata kusoma na kuandika akibahatika kuhudhuria shule. Sasa swali la kujiuliza ni kwamba mtoto anajifunza haya kutoka kwa nani?. Bila shaka ni kutoka kwa watu waliomzunguka, baba, mama, wakubwa zake ,majirani,ndugu, jamaa na marafiki ambayo hiyo tunaita jamii yake. Katika jamii hii atajifunza mazuri na hata mabaya yaliyopo ndani ya jamii yake. Bahati mbaya au nzuri ni kwamba katika kipindi cha kujifunza mtoto hawezi kuchagua cha kujifunza na cha kuacha kwani hana uwezo huo. Pia ni kipindi ambacho yeye huwa na uwezo mkubwa wa kuhifadhi vitu vingi na pia kuwa uwezekano mdogo wa kuyasahau. Hivyo basi chochote ambacho mto huyu atajifunza basi kitanasa kichwani kwa muda mrefu na kiasi kwamba anaweza kufikia umri wa utu uzima na bado akaendelea kukumbuka yaliyotokea utotoni. Hivyo basi malezi ya mtoto hasa katika kipindi chake cha udadisi ni cha muhimu na inabidi jamii yake iwe makini kwani ndicho kipindi ambacho wanaweza kumtengeneza raia mwema ama raia mbaya wa Taifa husika, kipindi ambacho chaweza kumjeruhi mtoto husika.

Kama nilivyotangulia kusema katika aya iliyotangulia ni kwamba mtoto hujifunza kila kitu kutoka kwa watu waliomzunguka (jamii na wazazi) hivyo basi mtoto hapaswi kulaumiwa kwa tabia aliyo nayo bali kufundishwa na kuonywa ama kuadhibiwa inapobidi. Ni rahisi zaidi mtoto kujifunza kwa kuona kuliko kuambiwa. Mathalani mtoto amelelewa katika mazingira ya ubabe halafu wazazi au walezi wake wanamwambia kwamba awe mpole, haiwezekani!. Hawezi kujifunza asichokiona, hajui upole unafananaje na una faida gani. Mzazi kutwa unashinda kutakana watoto wako wanapokosea halafu utegemee watoto wako wasitukane watakapokosewa, itakuwa ni jambo gumu sana kwake maana ndivyo alivyofunzwa kuishi.

Mzazi jitahidi kuishi yale maisha ambayo utataka mwanao aje kuyaishi. Kama unapenda wanao wapende kusoma, basi kuwa mfano bora katika kusoma na sio kuishia tu kuwaamrisha kusoma. Mtoto hajawahi kukuona unashika kitabu hata cha dini yako halafu yeye kutwa unamhubiria kufanya hivyo. Nakuhakikishia atachukua kitabu na kukikodolea macho, kuhesabu kurasa lakini kamwe hatasoma na ukitoka tu na yeye ataweka kitabu chini. Tusiigize maisha, kama unapenda kuangalia TV tegemea hilo kutoka kwa mwanao pia. Kwani hujawahi kusikia watu wakisema `mtoto wa fulani yuko kama baba ama mama yake?´ Ni kwamba tabia za watoto ni picha ya familia wanazotoka, ni mabalozi wa familia zao popote watakapokwenda. Usiwe tabia zile ambazo hupendi mwanao awe nazo na hazikuwakilishi vyema katika jamii.

Changamoto kubwa iliyopo pia ni wazazi kutingwa na kazi (busy) kiasi kwamba jukumu la malezi limeachwa kwa msaidizi wa ndani maarufu kama yaya ama Housegirl kwa kiingereza. Kama msaidizi huyo akiwa na tabia njema anaweza kulea vizuri lakini japo sio jukumu lake kulea muda wote. Yeye anapaswa kukusaidia tu katika kipindi ambacho haupo nyumbani. Ukirudi kutoka kazini mlee mwanao walau ajue kwamba wewe ni baba au mama, watoto wengine wamelelewa na wasaidizi kiasi kwamba humsahau mama na kudhani wale wasaidizi ndio mama zao na mama zao huwaita dada, msifike huko. Tekeleza jukumu lako kama mzazi na kama ukiona haupo tayari kulea basi usiwe na mtoto mpaka utakapokuwa tayari kulea. Kama msaidizi akiwa na tabia mbaya (wakati mwingine kutokana na anavyoftendewa na bosi wake) basi mtoto huuvuna huo ubaya maradufu na hata wakati mwingine kudhuriwa. Kwani kesi kama hizo hujasikia? Zipo nyingi tu siku hizi. Sisemi usiwe na msaidizi wa kazi, bali usimwachie yeye jukumu la kulea peke yake, hilo ni jukumu lako wewe mzazi (baba na mama).

Pia nitumie fursa hii kukukumbusha tena kwamba ufanye yale ambayo unaona yanafaa kwa mwanao na atajifunza kutoka kwako na atakuwa mtu bora na raia mwema. Tabia nyingi alizonazo mtoto amezipata kwenye jamii yake. Na kama mtoto wako ataanza kuwa na tabia ambazo huzipendi na wewe huzifanyi, tafuta chanzo cha tabia hizo mfano udokozi, matusi na tabia zinazofana na hizo na kumtenga na chanzo hicho kama hatua ya kwanza na pia kumkanya hata kumuadhibu pale inapobidi ili ajue kuwa kafanya kosa alijutie kosa hilo. Kwa wasomaji wa Biblia watakubaliana na mimi kuwa kuna mstari unaosema mlee mtoto katika njia impasayo naye hataiacha hata atakapokuwa mzee. Pia kuna msemo wa Kiswahili usemao mtoto umleavyo ndivyo akuavyo. Ukimlea vyema atakua vyema na ukimlea vibaya atakua vibaya. Usikubali mwanao awe balozi mbaya kwako na usiubali apatikane raia mbaya wa nchi yako. Jamii yetu isikae kimya na kushindwa kukemea mabaya ambayo wanayaona kwenye malezi ya watoto wa jamii zetu. Mke wa rais mstaafu wa awamu ya nne aliwahi kusema Mtoto mwenzako ni wako, na wa kwao pia ni wako. Kwa pamoja tuwalee ili tujenge taifa bora la sasa na la baadae. Mzazi usichukie pia pale mwanao atakapoonywa ama kuadhibiwa kwa makosa aliyofanya. Cha muhimu adhabu isiwe ndiyo kitu cha kukimbilia mtoto anapokosea, mpe elimu kwanza na akikaidi basi adhabu inayolingana kosa alilotenda itolewe. Usimlee kama yai,mlee kama mtoto. Kina baba jukumu la kulea ni la wazazi wote, baba na mama.
Mzazi, mlezi,ndugu jamaa, jamaa, marafiki na jamii kwa ujumla ni jukumu letu sote kulea na tunapaswa kulaumiwa sisi kwa tabia mbaya watakazokuwa nazo watoto waliopo katika jamii zetu.

Ni mategemeo yangu kwamba kwa pamoja tutajenga jamii imara na kuopata raia bora wa leo na hata kesho. Acha alama bora kwa mwanao ambayo kamwe haitafutika na atairithisha kwa wajukuu zako na hata kizazi chako chote.

Nina mengi ya kuandika lakini niishie hapa kwa leo. Tukutane katika makala zijazo, siku njema!.

Nickson Yohanes
nmyohanes@gmail.com
07538430303/ 0712843030

Je umepanda nini shambani kwako?

Habari za muda huu ndugu msomaji wa mtandao huu.
Kuna misemo mingi sana katika lugha ya Kiswahili na mmojawapo wa msemo huo ni memo usemao kwamba akipandacho mtu ndicho atakachovuna. Waliosema hivyo waliona mbali sana na msemo huu una ukweli ndani yake.


Kama swali lilivyouliza hapo juu ni dhahiri kwamba utavuna kitu chochote ambacho wewe utakuwa umepanda na sio vinginevyo na uzuri au ubaya wake ni kwamba utavuna maradufu. Mathalani ukipanda mbegu moja ya mwembe katika mazingira mazuri basi nayo itaota na kukupa idadi kubwa ya maembe. Je ukipanda maembe unaweza kutegemea kuvuna mapapai? Ama ukipanda maharage utavuna dengu? Jibu ni hapana utavuna sawa sawa na ulichokipanda wewe.

Nirudi kwenye swali la msingi sasa ni kwamba kila mtu anatakiwa kupanda kile ambacho atataka kukivuna baadae, mathalan kama unataka kupanda upendo huna budi kupanda upendo, kama unataka kupanda kuvuna amani huna budi kutenda haki katika maamuzi unayoyafanya. Hebu tuchukulie kwamba umepanda mbegu ya chuki hakika utavuna chuki maradufu. Huwezi kuvuna usichopanda hilo usilitegemee kamwe. Kama unataka kuwa tajiri huna budi kupanda juhudi na maarifa ambayo itaongeza thamani katika kile unachokifanya, na ukitaka kuwa na familia bora huna budi kuwekeza katika kupenda na kuijali familia yako. Kama unataka kupokea yakupasa pia kutoa, kama unataka afya bora huna huna budi kufuata kanuni bora za afya na mengine yahusuyo afya. Tatizo kubwa ambalo watu wengi wanalipata ni pale wanapoanza kupanda na kutegemea mavuno ya haraka katika muda mfupi tokea kupanda. Lazima usubiri kipindi cha mavuno kifike, mazao yako yakomae pia.

Labda nikuulize swali ndugu msomaji, mtu apandapo mahindi anaweza kuvuna ndani wiki? Ama apandapo minazi anaweza kupata nazi baada ya mwaka? Jibu ambalo nahisi utakuwa umelijibu ni kwamba haiwezekani na ni lazima kusubiri wakati unaendelea kutunza mazao yako shambani vile vile ndiyo hivyo utakavyoendelea kupalilia uyatakayo hata kama mazao bado hayaonekani. Hakuna mama anaetaka mtoto ambae atashindwa kusubiri miezi tisa, akishindwa kusubiri basi hatapata mtoto bali atapata njiti. Pia unatakiwa kupamda mbegu zako unazotaka kuvuna katika mazingira mazuri ambayo yataleta mazao mengi na bora. Mazingira hayo ni pamoja na kuwa na imani kwamba utavuna, kama huna imani kwamba utavuna hutakuwa na hamasa ya kutunza mimea yako.

Ndugu msomaji wangu nakushauri upande mazao bora tena ambayo utaweza kuvuna kwa muda mrefu japo yatahitaj pia muda mrefu kukua na kumea. Mkulima wa mchicha hupanda mbegu na kuvuna ndani ya muda mfupi lakini hataweza kuendelea kuvuna kwa kipindi kirefu, lakini mkulima wa minazi husubiri sana lakini siku akianza kuvuna atavuna kwa muda mrefu sana pengine kizazi hadi kizazi. Panda tabia njema na utavuna heshima, panda chuki na utavuna chuki, panda mema na utavuna mema, lea vizuri na tunza vyema familia yako na wewe utapata familia bora na yenye upendo, amani na heshima, saidia nawe utasaidiwa, hudumia nawe utahudumiwa. Watendee watu yale ambayo nawe utataka kutendewa na kamwe usimtendee mtu jambo ambalo wewe hutaki kutendewa. Kumbuka kila siku ni msimu wa kupanda.
Amua leo utapanda katika wema na wewe utavuna kwa wakati wake tena utavuna maradufu.

Nikutakie mafanikio tele.

Nickson Yohanes
0753843030 au 0712 843030

Je mtaji ni kikwazo kwako katika kuanza biashara au kuwekeza?

Ndugu msomaji wa mtandao huu wa PAMBAZUKA DAIMA natumaini upo salama na unaendelea vyema na mihangaiko yako ya kila siku. Kama wewe ni msomaji wa zamani utakumbuka kwamba nilikuwa naandika katika mtandao wa Life Adventures na kama wewe ni msomaji mpya basi karibu na pia nikujuze kwamba nimehamishia makala zote huku na nitakuwa naandika rasmi huku kama ilivyokuwa mwanzo japo kuna wakati nilisita kidogo kutokana na sababu zilizokuwepo juu ya uwezo wangu lakini sasa nimerudi tena kuendelea kukushirikisha kile ambacho mimi nakijua na pia kujifunza kupitia kwako kile ambacho nawe unakifahamu. Karibu kwa mara nyingine tena.


Baada ya utangulizi huo mfupi basi nianze makala hii fupi juu ya swali hapo juu. Watu wengi sana wamekuwa na kisingizio cha mtaji kuwa ndicho chanzo cha wao kushindwa kufanya biashara ama kuwekeza hata katika miradi midogo midogo, sipingani nao kuwa mtaji kwa watu wanoanza ni changamoto kweli. Lakini kukosa mtaji ni sehemu ndogo sana katika kuanza kile ambacho unataka kukifanya, tatizo kubwa hasa ni mtu kutokujua anatchotaka kukifanya na kukubali kuanza kidogo kidogo na kukua. Maana yake ni kwamba unaweza kuanza na kiasi kidogo ulicho nacho na kuendelea kuukuza mtaji wako kufikia kiasi ambacho unataka kuwekeza kama unataka kuwekeza kwenye biashara ama uwekezaji mkubwa.

Mtaji haujawahi kuwa tatizo katika kuanza kufanya biashara ama ujasiriamali. Tatizo hasa sio hilo bali ni tatizo kubwa ni wazo la biashara (business idea) kwa maana hata ukiwauliza watu ni kiasi gani cha mtaji kitawatosha wengi watashindwa kukuambia ni kiasi gani na kwani wengi hawajui wanataka hasa kufanya nini . Hata wale watakaoweza kukutajia kiasi basi utajikuta kuwa watataja kiasi kikubwa ambacho pengine itakuwa ngumu kwake kukipata kwa mara moja hivyo kuendelea kusubiri siku akipata huo mtaji ambao hakika haujui ataupata wapi na lini. Hivyo ukiangalia hapa ni lazima mtu awe anajua kwanza anachotaka kukifanya kabla hajapa mtaji wa fedha ambao ataweza kuuwekeza. Ni hartari sana kupata mtaji bila kujua unachotaka kukifanya. SOMA Makosa 10 ya kuepuka ili upate mafanikio ya kipesa

Kuna vitu vitatu ambavyo huwezi kuwa navyo kwa wakati mmoja. Kuna watu, wazo na mtaji. Maana yake unaweza ukawa na wazo na watu lakini ukakosa mtaji ama mtaji lakini huna watu ama huna wazo. Kwa maana hiyo basi ni itabidi uungane na mtu ambaye anacho unachokosa wewe. Kama huna mtaji lakini una wazo na mtaji basi mtafute mtu ambae ana mtaji na hana wazo la biashara (business idea) na mnaweza mkafanya jambo kubwa na mkafanikiwa sana na hivyo mtakuwa mmesaidiana na wote mtafaidika wote, wewe utakuwa umemsaidia mwenye hela wazo au watu na wewe umesaidiwa na mwenye pesa kuweza kupata mtaji. Watu wengi wamefanya hivyo na wengine wanaendelea kufanya hivyo. Cha muhimu na cha kuuzingatia ni kutafuta mtu alie tayari na pia mwaminifu.

Ukweli ni kwamba sio lazima uje na wazo jipya kama hutaweza kufanya hivyo, bali unaweza kuboresha mawazo yaliyopo na kutatua tatizo lilopo ambao waliokutangulia wameshindwa kuliona na kulitatua kwenye jamii yako. Angalia tatizo liliopo na kama ukija na utatuzi utakuwa umepata wazo la biashara na utakuwa umeanza safari yako ya kufanya biashara ama kuwekeza.
Natumaini utakuwa umeelimika na pia utachukua hatua. Usisite kutoa maoni yako na hata ushauri wako.

Nickson Yohanes
0753843030 au 0712843030
Ukiwa na hivi vitu vitatu utakuwa na maisha bora sana

Ukiwa na hivi vitu vitatu utakuwa na maisha bora sana

     Maisha ni jinsi unavyoyachukulia mwenyewe. Maisha bora unayaandaa mwenyewe. Kuwa na maisha bora na ya furaha kuna vitu ambavyo unatakiwa kuwa navyo. Vitu hivyo huwezi kuletewa na mtu yeyote isipokuwa wewe mwenyewe. Huhitaji pesa, umaarufu ama madaraka ili uwe na maisha bora na furaha. Simaanishi kwamba pesa, madaraka au umaarufu havihitajiki maishani la hasha, namaanisha kuwa kuwa navyo bila kufanya haya ni ngumu kuwa na maisha bora.
Kubadili vitu unavyoweza kubadili
Kubali usikubali kuna vitu ambavyo unaweza kuvifanya ama kuvibadili maishani, hivi vibadili haraka iwezekanavyo. Usisubiri aje mtu mwingine avibadili kwani mara nyingi vyote vipo ndani uwezo wako. Kubadili tabia zako hakuhitaji usaidizi wa profesa wako wa chuo, bosi wako wala mwenyekiti wako wa mtaa. Je huwezi kubadili tabia yako ya uvivu? Huwezi kubadili tabia yako ya ufujaji wa pesa? Huwezi kuamua kuwa na mafanikio? Huwezi kuwa mwekezaji? Bila shaka tabia hizo na nyinginezo nyingi ziko ndani ya uwezo wako na ukiamua kubadili hakika
Namna bora ya kupunguza uzito

Namna bora ya kupunguza uzito

Tatizo la uzito mkubwa limekuwa kubwa miongoni mwa jamii yetu. Tatizo hili linachangiwa kwa kiasi kikubwa na ulaji mbovu usiozingatia kanuni za afya. Kukubali kwamba una uzito mkubwa ni nusu ya kulitatua tatizo lako. Ili kujua kama una uzito mkubwa ni lazima uchukue kipimo kinachitwa
Makosa 10 ya kuepuka ili upate mafanikio ya kipesa

Makosa 10 ya kuepuka ili upate mafanikio ya kipesa


Pesa ni chombo kinachotumika kupima thamani ya vitu kama huduma na bidhaa. Pesa hutumika kubadilisha bidhaa na huduma mbalimbali. Kupata na kuhifadhi pesa imekuwa ni changamoto kubwa sana. Hivyo basi ili uweze kufanikiwa yakupasa kujifunza kuhusu pesa. Watu wengi waliofanikiwa wamejifunza na kuelewa pesa.


  1.  Matumizi yasizidi mapato
Ili uweze kufanikiwa kimaisha hasa katika suala la pesa, basi yakupasa kutumia pesa chini ya kiwango unachoingiza. Hii itakusaidia kuweka akiba kwa matumizi ya baadae na
Faida nne za ulaji wa chocolate

Faida nne za ulaji wa chocolate




Katika hali ya kawaida watu wengi wamezoea kusikia  na kuambiwa kuwa Chocolate si kitu kizuri na kuna sababu nyingi za kukufanya uamini kuwa chocolate si nzuri.
Watu husema inaharibu meno, wengine hudai kuwa inasababisha kisukari na wengine huenda mbali zaidi wakidhani kuwa inaharibu ngozi kutokana na wingi wa mafuta iliyo nayo.
Watoto wadogo ambao wamezoeleka kuwa wapenzi wakubwa wa chocolate ndio huvunjwa moyo na wazazi/walezi wao katika hili.

Madhara ya kuwa mdaiwa sugu



Katika maisha huwezi kupata kila kitu unachokitaka, pia huwezi kuhitaji kila unachokipata. Hakuna mtu yeyote duniani ambaye amejitosheleza kwa kila kitu na asihitaji msaada wa mtu mwingine yeyote, hata Billgates huhitaji msaada wa watu wengine ili aweze kuishi na kustawi katika maisha na biashara zake. Hakuna mtu yeyote ambaye anaweza kuishi maisha yake yote ya hapa duniani bila kukopa,hivyo basi kukopa sio jambo baya wala la ajabu. Jambo lililo baya ni kuwa mdaiwa sugu ama kutolipa madeni. Watu wengine hushindwa kulipa madeni si kwa sababu hawana uwezo wa kuyalipa bali hawaoni umuhimu ama hujisahau katika hilo.
Lengo la makala hii fupi ni
Jinsi ya kutengeneza maziwa ya soya nyumbani (soy milk)

Jinsi ya kutengeneza maziwa ya soya nyumbani (soy milk)

Utangulizi
Maziwa ya soya ni maziwa yanayotokana na mbegu za soya. Ni kinywaji kizuri kwa afya na pia hutumika kama kiburudisho. Maziwa ya soya hufanana sana na maziwa ya wanyama hasa ya ng’ombe katika virutubisho na pia mwonekano (rangi). Maziwa ya soya ni mazuri sana kwa sababu hayana lehemu (cholesterol),mafuta yasiyofaa/mgando (saturated fats) na yana virutubisho vingi. Maziwa haya hufaa sana pia kwa watu wenye mzio (allergy) na maziwa ya wanyama kutokana na kukosa kimeng’enyo kiitwacho lactose (lactose intolerant people).

 


Jinsi ya kuandaa
1)      Chambua soya zako kuondoa uchafu.
2)      Osha vizuri soya zako na maji safi.
Namna ya kuwa rafiki bora

Namna ya kuwa rafiki bora

Katika makala iliyopita tuliona jinsi marafiki walivyo muhimu katika maisha yetu. Hivyo basi leo nimeona ni bora nijaribu kueleza namna ya kuwa rafiki bora. Ili kuwa rafiki bora huna budi;
Umuhimu wa kuwa na marafiki

Umuhimu wa kuwa na marafiki


Pengine unaweza kujiulliza ni kwaninini nimeamua kuandika kuhusu umuhimu wa marafiki. Lakini mbali na hilo nikuulize una rafiki?  Najua unalijua jibu lako, lakini nisingependa uniambie. Najua kwamba unajua umuhimu wa marafiki ila nimeona nikukumbushe tu. Marafiki ni tunu kubwa tuliyonayo hapa duniani. Marafiki wanaweza kuwa chanzo cha wewe kufanikiwa ama kuporomoka katika nyanja mbalimbali. Kuna aina mbili za marafiki ambazo nitazitaja ni hapa ambazo ni urafiki wa karibu (close friends) na urafiki wa kawaida (acquaintances). Labda nianze na urafiki wa kawaida. Urafiki wa kawaida ni ule ambao mmekutana sehemu kama baa, kwenye michezo, muziki, sherehe au katika siasa na pia kwenye mitandao ya kijamii kama facebook. Urafiki huu hutokana na nyie kuunganishwa na kitu fulani. Mara nyingi urafiki huu ni wa muda tu na unaweza kuisha pale tu ambapo mtapoteza kile kitu kinachowaunganisha (common interest). Lakini aina ya pili ya urafiki ni ule urafiki wa karibu ambao unakuwa karibu na mtu,

Kanuni 7 za Uongozi bora

Uongozi ni kuonyesha njia kwa wengine. Uongozi thabiti huweza kushinda nyakati ngumu katika hii dunia, huku uongozi mbovu ukiitumbukiza jamii katika majanga na majuto. Dunia hii ishawahi kuwa na viongozi bora sana. Je unamkumbuka Abraham Lincoln, Mwl J.K. Nyerere, Sokoine, Mandela na wengi wengineo ambao wamekuwa mfano wa kuigwa vizazi kwa vizazi. Najua kuna wabovu pia ambao unawafahamu kuanzia ulimwengu wa kwanza mpaka wa tatu. Hayati Dr. Myles Munroe aliwahi kusema ‘jeshi la kondoo linaloongozwa na simba ni rahisi kulishinda kundi la simba linaloongozwa na kondoo’. Maana yake