Je mtaji ni kikwazo kwako katika kuanza biashara au kuwekeza?

Ndugu msomaji wa mtandao huu wa PAMBAZUKA DAIMA natumaini upo salama na unaendelea vyema na mihangaiko yako ya kila siku. Kama wewe ni msomaji wa zamani utakumbuka kwamba nilikuwa naandika katika mtandao wa Life Adventures na kama wewe ni msomaji mpya basi karibu na pia nikujuze kwamba nimehamishia makala zote huku na nitakuwa naandika rasmi huku kama ilivyokuwa mwanzo japo kuna wakati nilisita kidogo kutokana na sababu zilizokuwepo juu ya uwezo wangu lakini sasa nimerudi tena kuendelea kukushirikisha kile ambacho mimi nakijua na pia kujifunza kupitia kwako kile ambacho nawe unakifahamu. Karibu kwa mara nyingine tena.


Baada ya utangulizi huo mfupi basi nianze makala hii fupi juu ya swali hapo juu. Watu wengi sana wamekuwa na kisingizio cha mtaji kuwa ndicho chanzo cha wao kushindwa kufanya biashara ama kuwekeza hata katika miradi midogo midogo, sipingani nao kuwa mtaji kwa watu wanoanza ni changamoto kweli. Lakini kukosa mtaji ni sehemu ndogo sana katika kuanza kile ambacho unataka kukifanya, tatizo kubwa hasa ni mtu kutokujua anatchotaka kukifanya na kukubali kuanza kidogo kidogo na kukua. Maana yake ni kwamba unaweza kuanza na kiasi kidogo ulicho nacho na kuendelea kuukuza mtaji wako kufikia kiasi ambacho unataka kuwekeza kama unataka kuwekeza kwenye biashara ama uwekezaji mkubwa.

Mtaji haujawahi kuwa tatizo katika kuanza kufanya biashara ama ujasiriamali. Tatizo hasa sio hilo bali ni tatizo kubwa ni wazo la biashara (business idea) kwa maana hata ukiwauliza watu ni kiasi gani cha mtaji kitawatosha wengi watashindwa kukuambia ni kiasi gani na kwani wengi hawajui wanataka hasa kufanya nini . Hata wale watakaoweza kukutajia kiasi basi utajikuta kuwa watataja kiasi kikubwa ambacho pengine itakuwa ngumu kwake kukipata kwa mara moja hivyo kuendelea kusubiri siku akipata huo mtaji ambao hakika haujui ataupata wapi na lini. Hivyo ukiangalia hapa ni lazima mtu awe anajua kwanza anachotaka kukifanya kabla hajapa mtaji wa fedha ambao ataweza kuuwekeza. Ni hartari sana kupata mtaji bila kujua unachotaka kukifanya. SOMA Makosa 10 ya kuepuka ili upate mafanikio ya kipesa

Kuna vitu vitatu ambavyo huwezi kuwa navyo kwa wakati mmoja. Kuna watu, wazo na mtaji. Maana yake unaweza ukawa na wazo na watu lakini ukakosa mtaji ama mtaji lakini huna watu ama huna wazo. Kwa maana hiyo basi ni itabidi uungane na mtu ambaye anacho unachokosa wewe. Kama huna mtaji lakini una wazo na mtaji basi mtafute mtu ambae ana mtaji na hana wazo la biashara (business idea) na mnaweza mkafanya jambo kubwa na mkafanikiwa sana na hivyo mtakuwa mmesaidiana na wote mtafaidika wote, wewe utakuwa umemsaidia mwenye hela wazo au watu na wewe umesaidiwa na mwenye pesa kuweza kupata mtaji. Watu wengi wamefanya hivyo na wengine wanaendelea kufanya hivyo. Cha muhimu na cha kuuzingatia ni kutafuta mtu alie tayari na pia mwaminifu.

Ukweli ni kwamba sio lazima uje na wazo jipya kama hutaweza kufanya hivyo, bali unaweza kuboresha mawazo yaliyopo na kutatua tatizo lilopo ambao waliokutangulia wameshindwa kuliona na kulitatua kwenye jamii yako. Angalia tatizo liliopo na kama ukija na utatuzi utakuwa umepata wazo la biashara na utakuwa umeanza safari yako ya kufanya biashara ama kuwekeza.
Natumaini utakuwa umeelimika na pia utachukua hatua. Usisite kutoa maoni yako na hata ushauri wako.

Nickson Yohanes
0753843030 au 0712843030

Related Posts